Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambaye pia Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdallah Hamisi Ulega ameipongeza serikali ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kufanya kazi kubwa kuinua sekta ya elimu.
Akizungumza kwenye kongamano la Chama Cha Walimu Tanzania (CWT)kitengo cha wanawake Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani kongamano hilo lilofanyika kwenye ukumbi wa shule ya Mwinyi Sekondari. Mhe Ulega ameahidi kuchangia juhudi hizo kwa kutoa motisha mbalimbali.
Aidha aliwatoa hofu walimu hao kwa kuweka bayana kuwa Rais ataendelea kujibu kero katika bajeti ijayo huku Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Ras kutenga pesa za mapato ya ndani kuboresha miundombinu.
Mhe.Ulega aliwaomba walimu wafanye kazi ya ziada kuboresha matokeo ya wanafunzi kwenye mitihani ya Taifa hususani kufuta zero huku akikabidhi majiko ya gesi (200) kwa shule zote za Halmashauri hiyo na akiahidi kutoa mashine za kudurufu ( photocopy machine) kwenye kata nne za Halmashauri hiyo ili kila wiki wanafunzi wafanye mitihani ya majaribio kwa madarasa ambayo wanajianda na mitihani ya Taifa huku akikabidhi million mbili na nusu kama nauli kwa washiriki wa kongamano hilo.
Kwa upande wake Mtunza Hazina wa Taifa (CWT) Aboubakar Allawi ameungana na Mhe.Ulega kumpongeza Rais Samia huku Chama hicho kikiweka wazi kutambua juhudi za dhati katika kuboresha sekta ya elimu huku akimwomba msaidizi huyo wa Rais kufikisha kilio cha walimu kupanda madaraja.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.