Mbunge wa Jimbo la Mkuranga Mkoa wa Pwani ambae pia ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumwamini kwenye Baraza la Mawaziri huku akimtakia heri kwenye siku yake ya kuzaliwa .
Akizungumza kwenye halfa ya kukabidhi ng’ombe bora watatu na majokofu kwa vikundi vya wajasiriamali Wilaya za Mkuranga, Kibiti na Mafia kwenye ukumbi wa Flexi Garden Mkuranga Mhe. Ulega amewapogeza wafadhili ambao ni (WWF) kwa kutoa mashine ya boti na majokofu 8 sambamba na Mbogo Ranch kwa kukabidhi madume bora ya ng’ombe watatu.
Aidha Mhe.Ulega alitumia fursa hiyo kuahidi kuboresha wajasiliamali wa Samaki kwa kuwa na mkakati wa kuhamasisha uchumi wa bluu kwa kuleta neema kubwa kwenye mwambao wa Pwani wakishirikiana na (WWF).
Akitoa salamu za Serikali Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi,Khadija Nassir amempongeza Naibu Waziri kwa kuaminiwa na Rais kusimamia Sekta ya Mifugo na Uvuvi ambayo inagusa asilimia (70) ya wakulima na wafugaji. Bi Khadija amemuhakikishia Rais kusimamia na kutatua changamoto za wafugaji na wakulima .
Kwa upande wake Mwakilishi wa ( WWF) Dk.Modesta Medadi alisema wamejipanga kuwafikia wavuvi kwenye ukanda wa Pwani kwa kuwaletea vitendea kazi.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bi,Mwantum Mgonja amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa ataendelea kutimiza matwaka ya kisheria kwa kutenga asilimia kumi ya mapato ya ndani kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuwawezesha wajasiliamali huku akimpongeza kwa kuungana naye.
Akitoa shukrani zake Mwenyekiti wa Chama cha Wafugaji Wilayani Mkuranga Nata Mogeni amempongeza Mkurugenzi Naweed Mulla kwa kuwapa msaada wa majike bora ya ng’ombe .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.