Watoto wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa Pwani wamepata faraja kuelekea siku ya mtoto wa Afrika kufuatia mdau wa maendeleo kuikabidhi Halmashauri ya Wilaya magunia kumi ya mchele
Akiwakabidhi msaada huo juzi kwenye ofisi ya Halmashauri Mdau Ahmed Salum aliweka bayana amewalenga watoto ili kuwatia moyo katika changamoto mbalimbali wanazokutana nazo
Ahmed pamoja na kusema misaada hiyo ni endelevu alitumia fursa hiyo kuipongeza serikali kwa masuala ya sheria na sera kwenye ubakaji na kutoa adhabu ya kifungo miaka (30) au maisha kwa kosa la ubakaji ambalo waathirika wakubwa na watoto
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alishindwa kutafuna maneno kwa kumtaja Ahmed kuwa mfano wa kuigwa kufuatia michango yake mingi sekta mbalimbali
Munde aliyewakilishwa na mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii wa Halmashauri hiyo Peter Nambunga alipokea mchele huo sambamba na mabango makubwa matatu ya sherehe hiyo itayofanyika kijiji cha Bupu huku akimkabidhi barua ya shukrani
Nambunga alivitaka vikundi vya ujasiliamali vijiji mbali mbali vinavyofaidikaa na mikopo inayotolewa kwa wakati na Halmashauri ya wilaya kulenga zaidi miradi ya kilimo ambayo watoto watafaidika na uhakika wa chakula mashuleni pia majumbani
Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na mtunza hazina wa wa Halmashauri Medani Jekamaya sambamba na mratibu wa TASAF Safina Msemo aliyembatana na wataalamu mbalimbali .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.