Kamati ya Lishe Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani leo Mei 25,2022 imeketi kujadili taarifa za Robo ya tatu kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 kujadili taarifa ya utekelezaji wa shughuli za lishe ngazi ya kata na vijiji kwa kipindi cha Jan-Machi 2022.
Wakijadili mada tofauti zikizowasilishwa wakati wa kikao, Mganga Mkuu wa Wilaya Ali Mbikilwa amewaomba wana kamati kuwa mabalozi wazuri wa ulaji bora wa chakula huku ukizingatia mlo kamili.
Aidha Mkuu huyo alisema uamuzi wa ushirikishwaji wa Idara zote katika shughuli za Lishe umepelekea kufanya vizuri wakati walipokua wanapokea matokeo ya upimwaji katika kikao cha tathmini ya lishe robo ya pili na kupata ushindi kati ya Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Pwani.
"Kamati ya Lishe (W) sisi ndio wasimamizi wa shughuli za lishe ngazi ya kata kwa hiyo tuhakikishe mkataba wa lishe unafatwa kwa kata zetu zote 25" Alimalizia.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.