Mganga Mkuu Hospitali ya Wilaya Mkuranga Mkoa wa Pwani Dk. Ali Mbikilwa leo Mei,25, 2022 ameshiriki kikao kazi na viongozi wa vituo vya Afya vilivyopo ndani ya Wilaya.
Akizungumza na wataalam hao Dk. Mbikilwa amewapongeza kwa kukamilisha zoezi la chanjo kwa watoto 41083 na kuvuka lengo kwa kuwafikia watoto 44018 sawa na asilimia 107.14
Aidha Mganga Mkuu amewataka watumishi kwenye Vituo kuwahi kufika kazini na huduma za dharula kuendelea kutolewa hata baada ya muda wa kazi huku akiwataka watoa huduma kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi kulingana na kanuni na taratibu zote za afya.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.