Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Mnyeti amepongeza maandalizi yaliyofanywa kwenye maonesho ya nane nane kanda ya mashariki Mkoani Morogoro.
Amesema hayo leo tarehe 04/08/2024 alipotembelea kuona Teknolojia na bidhaa mbalimbali pamoja na vipando vya mbogamboga na malisho ya mifugo katika Banda la Mkuranga.
Mnyeti ametoa wito kwa taasisi za Serikali zinazoshiriki katika maonesho hayo kuleta vitu vizuri vya kuonesha katika mabanda hayo ili taasisi binafsi waige kwa Serikali.
Amesema ni vema kwa sasa wafugaji wote nchini kabla ya kuingiza mifugo sehemu yoyote atatakiwa kuonesha maeneo yake ya malisho ya Mifugo hiyo ili kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji.
Pamoja na hayo amepongeza kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kuandaa vipando vizuri vya Mifugo na kujianga vema katika Maonesho ya Mwaka huu sambamba na kutekeleza sera ya Serikali inayoongozwa na Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya uwekezaji kwa kuendelea kuongozeka kwa Viwanda Wilayani humo.
Akikagua bidhaa katika banda hilo amewataka wataalamu wa Kilimo na Mifugo kuhakikisha malisho yaliyopo katika bustani ya maonesho, iende ikatolewe elimu kwa wananchi wa Mkuranga ili nao waweze kufaidika na Teknolojia hiyo sambamba na kuwataka wananchi wafike Nane nane Kanda ya Mashariki kuja kujionea na kujifunza mambo mbalimbali badala ya kusubili kusimuliwa.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.