Mbunge wa Jimbo la Mkuranga ambae ni Naibu Waziri wa Wizara ya Uvuvi na Mifugo Mhe.Abdallah Hamis Ulega ameongozana na Viongozi wa CCM Mkuranga,Mwenyekiti wa Halmashauri,Mkurugenzi wa Halmashauri,Wataalam wa Wilaya,Wataalam wa Kata,Watendaji wa Vijiji na kufika katika mpaka wa Kata ya Mbezi na Kata ya Vianzi kwaajili ya kumkabizi mkandarasi Mradi wa barabara ya Vikindu na Ujenzi wa Kalavati kubwa katika barabaraba za Msorwa,Malela,Shungubweni na Marogoro.
Lengo la mradi huo ni kufungua mwasiliano ya barabara ili maeneo haya yapitike kipindi chote cha mwaka.Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi Nangara Traders Ltd ambao unagharimu kiasi cha Shilingi Mill.479,970,000.00 ambayo ni ruzuku ya serikali kupitia Tozo.
Mhe.Abdallah Ulega amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwakuweza kutupatia Billion 3 kwa Wilaya ya Mkuranga kwaajili ya kujenga madaraja na barabara zilizopo ndani ya wilaya yetu katika mwaka wa fedha 2022/20223.
Aidha amemtaka Mkandarasi Nangara Traders kuwa na ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wa kata zote mbili pamoja na wananchi wake na amewataka wananchi wawe kipaumbele cha kwanza cha kulinda vifaa vitavyokuwa vinatumika katika mradi huo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.