Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe Deogratius Ndejembi amewaasa watumishi Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani kuacha kufanya kazi kwa mazoea.Akizungumza nao juzi kwenye ukumbi wa Flexi uliopo Kiguza Ndejemi ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma alisema malipo pekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa utamaduni wake kuwajali watumishi ni kufanya kazi kwa bidi.
Aidha kiongozi huyo aliwageukia watumishi wa idara ya Ardhi akiwataka wabadilike na kukomesha migogoro ya Ardhi sambamba na kuandaa maeneo ya Ardhi kwa uwekezaji hatimaye mapato ya serikali yaongezeke na kupanua soko la ajira.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi.Mwamtum Mgonja kutenga bajeti kwa ajili ya watumishi kujiendeleza kielimu likizo sambamba na kuiwezesha wataalamu wa idara ya utumishi kwenda Makao makuu Dodoma kufatilia changamoto mbalimbali za Watumishi zikiwemo mabadiliko ya mishahara baada ya kupanda madaraja ,madeni mbalimbali.
Akitoa salamu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mikakati yake ya kuondoa malalamiko ya Watumishi huku akimhakikishia Naibu huyo kuwa wao hawana likizo yeyote wanashirikiana kufanikisha ujenzi wa madarasa kupitia fedha za (uviko 19) lengo wanafunzi wawe madarasani wote shule zikifunguliwa .
Kwa upande wake Mkurugenzi Bi.Mwamtum Mgonja alimuomba kiongozi huyo kuwalipa malimbikizo ya mishahara Watendaji wa vijiji 56 ambao serikali iliwarejesha kazini kwani madai yao ni ya muda mrefu na wanakaribia kustaafu.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Mhe Deogratius Ndejembi amewaasa watumishi Wilayani Mkuranga Mkoa wa Pwani kuacha kufanya kazi kwa mazoea.Akizungumza nao kwenye ukumbi wa Flexi uliopo Kiguza Ndejemi ambaye pia Mbunge wa Jimbo la Chamwino Mkoani Dodoma alisema malipo pekee kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa utamaduni wake kuwajali watumishi ni kufanya kazi kwa bidi.
Aidha kiongozi huyo aliwageukia watumishi wa idara ya Ardhi akiwataka wabadilike na kukomesha migogoro ya Ardhi sambamba na kuandaa maeneo ya Ardhi kwa uwekezaji hatimaye mapato ya serikali yaongezeke na kupanua soko la ajira.
Aidha alimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri Bi.Mwamtum Mgonja kutenga bajeti kwa ajili ya watumishi kujiendeleza kielimu likizo sambamba na kuiwezesha wataalamu wa idara ya utumishi kwenda Makao makuu Dodoma kufatilia changamoto mbalimbali za Watumishi zikiwemo mabadiliko ya mishahara baada ya kupanda madaraja ,madeni mbalimbali.
Akitoa salamu Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally alimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa mikakati yake ya kuondoa malalamiko ya Watumishi huku akimhakikishia Naibu huyo kuwa wao hawana likizo yeyote wanashirikiana kufanikisha ujenzi wa madarasa kupitia fedha za (uviko 19) lengo wanafunzi wawe madarasani wote shule zikifunguliwa .
Kwa upande wake Mkurugenzi Bi.Mwamtum Mgonja alimuomba kiongozi huyo kuwalipa malimbikizo ya mishahara Watendaji wa vijiji 56 ambao serikali iliwarejesha kazini kwani madai yao ni ya muda mrefu na wanakaribia kustaafu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.