Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amehudhuria Mkutano wa kufafanua Miongozo ya uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari Mwaka 2022 katika ukumbi wa Ujenzi Sekondari.
Katika Mkutano huo umeuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga,Makamu Mwenyekiti wa Halmshauri,Katibu wa CCM (Mkuranga),Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri,Mwenyekiti huduma za jamii,Wakuu wa idara elimu msingi na sekondari,Maofisa elimu msingi na sekondari,wadhibiti ubora,Maafisa elimu Kata,Wakuu wa shule msingi na sekondari.
Katika Mkutano huo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amesema walimu wanatakiwa kupunguziwa majukumu haswa ya kusimamia miradi ya elimu kwani hupoteza muda mwingi katika usimamizi wa miradi hiyo na wanafunzi kukosa huduma stahiki hvyo basi walimu waendelee na majukumu yao ya kazi ili wanafunzi wasikose Huduma wanazopata.
Aidha amezungumzia lishe bora kwa watoto na kuagiza shule zote za msingi na sekondari zianzishe mashamba darasa na skimu za umwagiliaji ili kupunguza njaa kwa wanafunzi na akaweka bayana kutotoa tena vibali vya kuchangisha chakula mashuleni.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi.Mwantum Mgonja amewataka walimu wawe na nidhamu katika vituo vya kazi na kusisitiza kuishi karibu na vituo vya kazi ili waweze kutoa huduma kwa wakati sahihi kwa wanafunzi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.