Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mh. Hadija Nasri Ali ameshiriki kwenye kikao kazi cha mradi wa kufufua zao la korosho Wilaya ya Mkuranga kilicho andaliwa na Taasisi isiyo ya Kiserikali Mwambao Aglicuture Development Organization (MWADO) kikiwa na lengo la kuhamasisha upandaji wa mikorosho mipya sambamba na uanzishaji wa mashamba mapya ya Mikorosho.
Aidha Taasisi hiyo imelenga kutoa mafunzo ya mara kwa mara kwa wakulima wa korosho huku ikihamasisha kuongeza mnyororo wa thamani wa zao la Korosho ghaf,Sambamba na kutoa elimu kwa wananchi ya kuanzisha viwanda vidogo vya ubanguaji.
Taasisi ya MWADO ilianzishwa mnamo mwaka 2012 na kupata usajili 2013 ambapo sehemu kubwa ya wanzilishi ni watanzania kutoka Wilaya ya Mkuranga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.