Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.KHadija Nasri Ally amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kwa kuleta fedha za ujenzi wa madarasa.
Akitoa salamu za serikali katika mkutano maalum wa Baraza la madiwani ulioketi kujadili taarifa za fedha za Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa mwaka wa fedha ulioisha tarehe 30 Juni 2022 alitumia fursa hiyo kuwapongeza Madiwani kwa kazi nzuri ya kusimamia kazi za maendeleo.
Akizungumzia changamoto za wakulima ambao wanachangia asilimia 70 ya mapato ya Halmashauri na kumuagiza kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha mapato yanatumika kuboresha miundombinu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhe.Mohamedi Salum Mwera aliungana na Kamisaa wa Wilaya kumpongeza Rais kwa kuwarahisishia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kufuatia utamaduni wake kuleta pesa kila mara za miradi ya maendeleo katika sekta mbalimbali.
Akiwasilisha taarifa ya fedha mwaka 2020-2021 Mtunza Hazina wa Halmashauri Bw.Patrick Magehema amesema wamekusanya kiasi cha Bil.7.416 huku mwaka 2021-2022 wameongeza hadi kiasi cha Bil.9.315.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtenda Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwanamsiu Dossi alliwahakikishia Madiwani na wananchi kwa ujumla baada ya mawasiliano ya pesa kutumia mfumo wa kimataifa watajikita kutoa elimu kwa Madiwani ili wawafafanulie wananchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.