Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake Wilaya ya Mkuranga Amina Abdalla (ambaye pia ni Mke wa Mbunge wa Jimbo la Mkuranga) jana ameongoza harambee katika Kijiji cha Makumbea Kata ya Magawa na kufanikisha kupatikana mifuko 100 ya saruji ambayo itatumika katika kuanzisha ujenzi wa Zahanati mpya ya Kijiji hicho.
Aidha katika harambee hiyo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Magawa Mh. Juma Abeid aliwahasa wananchi wa Kijiji cha Makumbea kujitoa kwa hali na mali ili kufanikisha ujenzi wa Zahanati hiyo na kuwaonya kuwa pamoja na serikali kutoa fedha za ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini ni lazima na wao wajitoe kwa hali na mali katika kile kidogo wananchopata katika shughuli zao zinazowaingizia kiapato.
Akijibu swali lililoulizwa kuhusu miundo mbinu ya barabara, umeme na mawasiliano Mh. Abeid amesema kwa upande wa Barabara wananchi wawe wavumilivu kusubili mvua zipite kwani tayari wameshapata kiasi cha shilingi Milioni mia moja na kumi (Mil. 110,000,000/=) kwa ajili ya ujenzi na uboreshaji wa Barabara hizo, kwa upande wa umeme Kata ya Magawa imeshaingizwa katika mpango wa awamu ya tatu kwa kanda ya Kibiti na wakati wowote wataanza kuchimbia nguzo na hatimaye kupata umeme.
Nae Mhandisi msaidizi Wilaya ya Mkuranga Bujiku paul aliwaambia wanakijiji kuwa wako nao bega kwa bega katika kusimamia Zahanati hiyo kuanzia uchoraji wa Ramani utakaokidhi matakwa ya majengo ya Serikali sambamba na kuishirikisha idara ya ujenzi katika kila hatua ya ujenzi huo ili kuwa na jengo lenye ubora.milioni
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.