MIKOKO DEVELOPMENT FOUNDATION ikishirikiana na Taasisi ya WWF imetoa vifaa vya kuwezesha kitalu miche kilichopo katika eneo la Msitu wa Vikindu ambacho kitaweza kuongeza uzalishaji wa miche ipatayo elfu 20 katika kipindi cha mwaka 2022.Vifaa hivyo vilivotolewa ni vikiwemo ndoo za kumwagilia maji (water can),tolori la kubebe udongo,viriba vya kupandia miti kilo 110,mabuti,makoti,visu,majembe,mikasi pamoja na makoleo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mikoko Development Foundation Bw.Olais Raphael amesema Tumejipanga kuleta mabadiliko katika Wilaya ya Mkuranga kwani ina utalii mzuri wa ndani kwa kupitia Msitu huu wa Vikindu kitalu hicho kitachoandaliwa kitaweza kuwa fursa nzuri kwenye sekta ya utalii na kuwa kivutio cha utalii na pia wananchi haswa vijana kuweza kujifunza na kuweza ikiwa pamoja na lengo letu ambalo tunataka kuanzisha club mashuleni na kufanya shule zote za Wilaya Mkuranga kupendeza na kuwa rangi ya kijani.
Aidha lazima tuwe na mikakati ya pamoja ambapo tunamshukuru sana Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwamtum Mgonja kwa kuweza kutenga bajeti kwaajili ya Kitalu hicho na kuweza kutupa zaidi hamasa kwa sisi kama Taasisi kuweza kuzidi kuleta michango yetu
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.