Halmashauri ya Mkuranga imeendesha mafunzo ya siku moja kwa vikundi vya ujasiliamali 19 vinavyotarajiwa kupewa mkopo wa asilimia 10 ambapo mil 155 zinatarajiwa kutolewa awamu ya pili kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.
Akizungumza wakati wa mafunzo hayo afisa tarafa Mkuranga Clement Muya kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amewapongeza Idara ya maedeleo ya jamii wilayani humo kwa kutoa elimu hiyo na kuwataka wajasiliamali kutumia mkopo watakao upata kwa malengo yaliyokusudiwa ili uweze kuwanufaisha
Aidha Muya amewataka wataalamu mbali mbali ngazi zote kuwafatilia na kushirikiana na wajasiliamali hao kwa kuendelea kuwasimamia kwenye kazi zao ikiwemo idara ya kilimo na mifugo kwa kuwapa elimu ili kuleta tija katika kazi zao wanazozifanya ili waondokane na umasikini.
Naye Peter Nambunga Afisa Maendeleo ya jamii wilaya amesema Halmashauri inatarajia kutoa zaidi ya mil 600 kwa mwaka wa fedha 21/22 kwa wajasiliamali hivyo amewataka kurejesha fedha wanazokopeshwa ili wengine nao waweze kukopa.
“Wanakutana na changamoto kubwa ya ulipaji wa marejesho kwa wakati na hii ni kwa sababu wajasiliamali wamekua sio watu wa kutimiza wajibu wao mpaka wafatiliwe kuhimizwa kurejesha marejesho”.Alisema Nambunga
Sambamba na hilo Afisa Takukuru aliyehudhuria mafunzo hayo Bi. Afsa kitime ametoa wito kwa wale wanaoshughulikia upatikanaji wa mikopo kuhakikisha wanafuta sheria na taratibu za utoaji wa mikopo ili kuepuka mazingira ya rushwa.
Wakizungumza kwa niaba ya wenzao wajasiliamali hao wamefurahishwa na mafunzo hayo na wameshukuru na kuahidi kutumia mikopo hiyo vizuri ili iweze kuwainua kiuchumi na hatimae maisha yao na familia zao kuboreka.
Aidha katika kuhakikisha fedha za mkopo zinatolewa na zinakua salama Kaimu Mwanasheria wa Halmashauri ya Mkuranga bi. Mary Kavile amewasainisha mkataba juu ya matumizi ya fedha hizo kwa vikundi vyote 19.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.