Serikali imerejesha utoaji wa Mikopo kwa vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu kuanzia Julai 2024.
Maelekezo ya Serikali kuhusu utoaji na usimamizi wa Mikopo inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa makundi hayo yameshatolewa na sasa Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendelea kukamilisha nyaraka mbalimbali za usimamizi wa mfumo wa utoaji na usimamizi wa mikopo hiyo baada ya kuboreshwa.
Hayo yamebainika katika kikao cha robo ya nne ya Mwaka wa fedha 2024/2025 cha Kamati ya Mikopo Wilaya ya Mkuranga kilichofanyika tarehe 21 Agosi 2024 kwenye ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri baada kupokea barua ya maelekezo hayo kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi.
Akifunga kikao hicho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Waziri Kombo ambaye ni mwenyekiti wa kikao hiko amesema hatokubali kuona mikopo hiyo wanapewa watu vikundi ambavyo haviko tayari kurejesha mikopo hiyo kwani kufanya hivyo kutasababisha wananchi wengine kukosa fursa ya kukopa.
Aidha kamati ya mikopo ngazi ya Wilaya itaendelea kufuatailia madeni kwa vikundi na watu wanaodaiwa marejesho ya mikopo sambamba na kutoa wito kwa viongozi wa vijiji kutoa ushirikiano mkubwa wakati wa ufuatailiaji wa madeni hayo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.