Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Eng.Mshamu Munde Leo amehitimisha mafunzo ya siku mbili kwa vikundi vya ujasiriamali vya wanawake na Vijana katika kata ya Kimanzichana.
Akiongea wakati wa kufunga mafunzo hayo Eng Munde alisema lengo la kutoa mafunzo hayo ni kuhakikisha kwamba Fedha zinazokopeshwa na Halmashauri zinatumika kulingana na mahitaji halisi ya kikundi lakini pia kuendeleza biashara na kurejesha mikopo ili vikundi vingine vipate fursa ya kukopa.
Eng Munde aliongeza kwa kusema changamoto ya masoko ya mananasi na mapesheni imeisha sababu kuna wadau wamejitokeza kuanzisha kiwanda "Tumepata wadau ambao wako tayari kuanzisha kiwanda na hivyo wameomba kununua mananasi na mapesheni hivyo bidhaa hizi hazitaharibika tena, pia nawasihi muendelee na Kilimo hiki zaidi"
Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Mkuranga ndugu Peter Nambunga alisema mafunzo haya hufanyika kwa wanavikundi vya ujasiriamali vya wanawake na vijana kila wanapotaka kutoa mikopo kwa lengo la kuwaelimisha namna ya kutumia fedha walizoomba kwa ajili ya biashara zao lakini pia kuwasaidia namna ya kupata masoko.
Bi joyce philipo mwanakikundi wa VEPAMO women group wanajishuhulisha na uuzaji wa nguo za wakina mama alisema "mafunzo haya yamenisaidia kufahamu nani ni soko kumbe soko ni mteja ambae anayekuja kununua bidhaa zangu lakini pia nimejifunza kujiamini katika biashara yangu".
Bwana Shaweji Mohammed Mwenyekiti wa kikundi cha Kazi Kwanza ambapo wanajishughulisha na ulimaji wa mananasi na mpaka sasa wamelima mananasi ekari 15 na wanashukuru kwa kauli ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mkuranga kupata wawekezaji ambao watanunua mananasi kutoka kwao hivyo bidhaa zao hazitaharibika.
Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa kata 15 kati ya kata 25 ambazo ni Mkuranga, Mkamba,Magawa, Kimanzichana, Mwarusembe, Nyamato, Lukanga, Njianne, Kisiju,Kiparang'anda, Vikindu, Vianzi, Mipeko, Tambani na Mwandege.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.