Kiasi cha shilingi Milioni tisa Laki saba na ishirini na nne elfu (9,724,000/=) kimetolewa kwenye vikundi vya watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa kugawa 2% ya mapato ya ndani ya Halamashauri ya Wilaya ya Mkuranga.
Akiongea wakati wa ugawaji wa fedha hizo Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga, Stephen Mwandambo amesema wanavikundi wasibweteke kwa kutumia fedha walizopewa kwenye matumizi yao binafsi na badala yake watumie katika malengo waliyoyapanga ili waweze kufanya marejesho hatimaye fedha hizo ziweze kutumika katika vikundi vingine.
Aidha afisa ustawi Neema Nyasulu amesema, wao wamejipanga kikamilifu katika kufuatilia fedha hizo na shughuli zote ambazo vikundi vitatekeleza kutokana na fedha hizo na hatimaye kuleta matokeo chanya
Nae Hamisi Mtango Ambaye ni mnufaika ameishukuru Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwa kutekeleza agizo la Serikali la kutenga 10% ya mapato yao kwa ajili ya kukopesha fedha hizo katika vikundi mbalimbali bila riba ilikiwepo la walemavu.
Jumla ya vikundi vitatu (3) vimefanikiwa kupata fedha hizo ambavyo ni kikundi cha umoja wa walemavu Kisemvule (UWAKI) wamepata shilingi Milioni 5,724,000, Upendo Group shilingi 2,500,000 na kikundi cha Amsha Amsha 1,500,000.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.