Mkuu waWilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mh. Filberto Sanga amewataka wananchi kujenga tabia ya kupanda miti katika maeneo wanayoishi ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kusababishwa na uharibifu wa mazingira kutokana na mabadiliko ya hali ya tabia Nchi
Sanga aliyasema hayo wakati akihutubia hadhara katika viwanja vya shule ya msingi chatembo wakati wa maadhimisho ya siku ya upandaji miti ambapo alisema hili ni agizo linalotekelezwa kutokana na waraka uliotolewa na Serikali wa kuwataka wanachi wote kushiriki siku ya upandaji miti kitaifa kila mwaka ili kupunguza madhara yanayotokana na uvunaji wa miti kwa ajili ya shughuli za binadamu .
“Maamuzi ya kupanda miti kila mwaka yamefikiwa baada ya kuona misitu katika nchi yetu inatoweka kutokana na shughuli za kila siku za kibinadamu hasa matumizi yanayozidi uwezo wa misitu yetu kujizalisha hali hii imesababisha maeneo mengi kupata athari zitokanazo na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo joto, mafuriko, vimbunga” alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema kwa taarifa iliyopo utendaji wetu sio mbaya kwa kuwa vitalu vya vikindu na kibiti vinasaidia kwenye kutimiza malengo hayo ya kuzalisha miche mbalimbali ya miti
Sambamba na hilo, Munde alisema “natambua pia kuna changamoto za wananchi wa kawaida kutojihusisha na upandaji wa miti hususani isiyokuwa ya matunda”
Aidha, aliendelea kusema kuwa umuhimu wa misitu ni mkubwa sana sisi kama Wilaya tumejipambanua kwa sababu tuna viwanda vingi sana lakini shughuli za viwanda zinaenda Pamoja na uzalishaji wa hewa taka na sio tu kwa sababu ya shughuli zao lakini ni Pamoja na uwingi wa watu wanaofanya kazi katika viwanda hivyo, hivyo basi ni muhimu kuendelea kupanda miti ili kusaidia kurekebisha hali ya hewa na kupunguza athari za hewa chafu inayotokana na uwepo wa viwanda.
Katika maadhimisho hayo watu binafsi na Taasisi mbalimbali vimehamasishwa kutumia fursa iliyotolewa na mfuko wa misitu Tanzania (TaFF) kuandika miradi ya hifadhi za misitu na ufugaji wa nyuki na kuwezeshwa.
Msitu wa Vikindu,kwa sasa unatumika kuingiza kipato kwa shughuli za utalii ikologia, ambapo watalii 161 wa ndani na wa nje wametembelea kivutio hiki kilichokuwa kichaka cha kujificha wahalifu na eneo la uvunaji haramu wa mazao ya misitu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.