Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga na Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani zimeadhimia kutengeneza kiungo (link) cha ushirikiano katika sekta ya utalii ili iwe rahisi kuifanya sekta hiyo kuongeza ufanisi wenye tija katika kukusanya mapato yatakayosaidia serikali kufikia uchumi wa kati.
Maadhimio hayo yalifikiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani Kanali Emmnauel H.Mwaigobeko na Timu ya utafiti wa fursa za utalii – Mkuranga iliyotembelea Mkoani Mtwara kwa lengo la kujifunza na kuangalia namna ya kuboresha vivutio vyake katika vya Utalii
Mwaigobeko alisema endapo kutakua na mashirikiano mazuri baina ya Halmashauri hizo mbili itakua ni fursa kwa watalii wanaotembelea Mtwara kufika Mkuranga na wanaofika Mkuranga kufika Mtwara pia jambo litakalozinufaisha Halmashauri zote mbili kimapato lakini pia itawashibisha watalii kwa vivutio vinavyopatikana sehemu hizi mbili.
Naye kiongozi wa Timu hiyo ya Utafiti kutoka Wilayani Mkuranga, Ndugu Pembe Mlekwa ambaye pia ni Afisa Michezo na Utamaduni wilaya ya Mkuranga alisema, serikali imesisitiza Halmashauri zote nchini kutambua na kuboresha vivutio vyake vya utalii, hivyo katika kutekeleza agizo hilo wamependelea kujifunza Mtwara na Kilwa – Lindi kwani ni moja kati ya mikoa iliyopiga hatua katika sekta ya utalii
Timu hiyo ya watafiti imeweka kambi ya muda mfupi katika Manispaa ya Mtwara - Mikindani na kufanikiwa kutembelea Vivutio kadhaa ikiwemo “The Old Boma” pamoja na fukwe ya Makonde (Makonde Beach) wakati ikijipanga kutembelea katika mji wa Kilwa kwa lengo la kujifunza na kupanua wigo wa ushirikiano katika sekta ya utalii.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.