Baraza la Madiwani Mkuranga limepitisha maombi ya Kampuni ya Tanzania Commodity Commerce and Investment LTD ya utiaji saini hati ya makubaliano ya ushirikiano na Halmashauri ya Mkuranga katika mradi wa uwekezaji wa Kilimo cha kaaba kwa zao la Muhogo
Kampuni hiyo imetenga Dollar za Kimarekani Milioni Hamsini kwa uwekezaji wa awali ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania Bilioni 125,000,000,000.
Mkutano huo ukiwa wa robo ya nne ya Mwaka wa Fedha 2023-2024 umefanyika jana kwenye ukumbi Flex Garden Kiguza.
Akitoa salaam za Chama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mkuranga Mh. Juma Magahila ameshukuru na kupongeza kwa kupatikana kwa kampuni hiyo ya kuchakata mihogo kwani itaenda kuongeza mnyororo wa thamani katika zao hilo na kuongeza kipato kwa wananchi wa Mkuranga.
Nae Katibu Tawala Wilaya ya Mkuranga Omari Mwanga amewataka viongozi kuhakikisha fedha zote za Serikali zikasimamiwe vizuri na zikatumike kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa katika kuendeleza miradi ya maendeleo.
Aidha amekataza kesi za ulawiti na ubakaji kumalizwa kwa ngazi za familia badala yake ametaka jamii zikae na kutafuta njia na namna ya kuzua uhalifu huo na ikishindikana basi taarifa hizo zifike sehemu husika kwa hatua zaidi.
Akifunga Mkutano huo Mwenyekiti wa Baraza hilo Mh. Mohamedi Mwela amempongeza Mkurugenzi Mtendaji na wataalamu wake kwa kufanikisha kukusanya mapato kwa zaidi ya lengo lililokusudiwa na kuyatumia vizuri sambamba na kuwapongeza viongozi wa CCM kwa malezi na kuwasimamia vema bila kusahau viongozi wa Ulinzi na Usalama kwa kutoa ushirikiano mkubwa katika kipindi chote cha zoezi la kukusanya mapato ya Halmashauri
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.