Kundi la sanaa na maigizo “Mkuranga Mpya” limefanikisha siku ya mazingira duniani iliyofanyika kiwilaya kijijini Mwanambaya kufuatia maonesho yao yaliyochangia wananchi wafahamu athari za mifuko ya plastiki.
Wakiigiza mbele ya mgeni rasmi Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Juma Abeid wasanii hao chipukizi walikonga mioyo ya washiriki baada ya igizo lao linalolenga wananchi watambue serikali imejipanga kuwa na mifuko mingi mbadala yenye bei nafuu
Kivutio kikuu ni pongezi zao kwa Halmashauri ya Wilaya chini ya Mhandisi Mshamu Munde kwa kutumia wiki kuhamasisha madhara ya mifuko hiyo huku wakiomba elimu hiyo iwe endelevu kwenye vitongoji na Vijiji.
Akiwaongoza wasanii hao kwenye zoezi la kukusanya mifuko hiyo hatarishi kwenye maeneo mbalimbali kijijini hapo, Mwenyekiti wa kamati ya uchumi, ujenzi na mazingira Halmashauri ya wilaya Shabani Manda aliwahakikishia waigizaji hao mahiri kwenye kampeni ya wilaya “Tokomeza mifuko ya Plastiki” ili jamii kiujumla iwe na uelewa.
Manda mwenye taaluma ua uandishi wa habari ambaye pia ni Diwani wa kata ya Tengelea alitumia fursa hiyo kumuagiza Afisa Mazingira wilaya Herman Basisi kuwaalika wamiliki wa Viwanda, Taasisi mbalimbali na wenye mashimo ya mchanga ili wabadilike hatimaye kampeni ya tokomeza mifuko ya plastiki ifanikiwe.
Hafla hiyo iliyoambatana na upandaji wa miti, ilifungwa na Mwenyekiti wa Halmashauri amabaye ni Diwani wa kata ya Magawa (CCM) aliyewaagiza Wataalam Watendaji kata zote (25) kushinda kwenye Vitongoji kuhamasisha Vikundi vya ujasiliamali kubuni miradi ya kutengeneza mifuko ya mbadala wajikwamue kiuchumi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.