Mkuu wa Wilaya ya Mafia Aziza Ally Mangosongo akiwa na wajumbe wake wa Kamati ya Usalama wamefanya ziara ya kutembelea eneo la Dindini Kisiju Pwani Wilaya ya Mkuranga.
Kamati hiyo imefanya ziara hiyo ya kikazi jana tarehe 26 Juni 2024 ikiwa na lengo la kuona eneo ambalo linatarajiwa kujengwa Bandari ambayo itaweza kuboresha utoaji wa huduma ya usafirishaji kwa wananchi.
Mwenyeji wa ziara hiyo Khadija Nassir Ali ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
amesema Bandari ya kisiju imekuwa na changamoto ya kuwa na matope ambayo yanatokana na maji ya Mito inayozunguka Bandari hiyo na kupelekea kuleta changamoto katika usafirishaji abiria.
Pia amesema vimefanyika vikao mbalimbali vya Majadiriano pamoja na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ili kuona namna ya kuweza kuboresha bandari hiyo.
Aidha ameomba kuungana kwa kamati zote mbili za Usalama ya Wilaya ya Mkuranga na ile ya Wilaya ya Mafia ili kuweza kufanikisha jambo hilo litakalokwenda kuondoa changamoto ya Usafiri kwa Wananchi wanaotumia usafiri wa majini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.