Madiwani wanaounda Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani wameombwa kuwaagiza Wenyeviti wa vitongoji na vijiji sambamba na watendaji wao ili wahamasishe wananchi wafurike kwenye kijiji cha kipala mpakani kuupokea mwenge wa uhuru kimkoa jumatano.
Akizungumza ofisini kwake jana Mkuu wa Wilaya Filberto Sanga alisema zitakuwepo Burudani mbali mbali kwa ajili ya Mkesha ili kuamkia mapokezi ya Mwenge toka Mkoa wa Dar es salaam .
Aidha Sanga aliwageukia Madiwani Wenyeviti ,Watendaji sambamba na Walimu ambao kuna miradi ya Mwenge wahakikishe wananchi wanakuwepo kwa wingi kwenye matukio huku wakijipanga kwenye suala zima la ulinzi na usalama.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alitumia fursa hiyo kuwataka watendaji wataalamu na Wakuu Wa Idara kuhakikisha wanakuwepo kwenye matukio na hususani salam za utii kwa Raisi Dk. John Pombe Magufuli, na mkesha kuelekea kukabidhi kwa kishindo Mwenge Wilaya ya Kibiti kijiji cha Jaribu Mpakani.
Naye mdau maarufu Ahmed Salim wa kijiji cha Kisemvule aliwataka wananchi wenzake waupe umuhimu Mwenge wa Uhuru ulioasisiwa na BABA WA TAIFA hayati Julius Nyerere huku akiwaomba wananchi wa kata ya Vikindu kuwahi mapema asubuhi ya Jumatano na Alhamisi ili kuupokea na kusindikiza kwenye wilaya YA KIBITI .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.