Serikali ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani imekabidhi madawati (122) kwa wanafunzi wa shule ya sekondari Mwinyi kama alivyoagiza Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliposimama Wilayani humo akitokea masasi kumzika Rais mstaafu awamu ya tatu hayati Benjamin Mkapa.
Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika jana shuleni hapo, Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga pamoja na kumpongeza kiongozi huyo wa Taifa kwa mikakati yake ya kuboresha sekta mbali mbali ikiwemo elimu kupitia mapato ya ndani alisema katika kuunga mkono jihudi hizo wamejiongeza na kuanza ujenzi wa matundu ya vyoo kwa shilingi milioni tatu.
Aidha sanga aliwataka wanafunzi hao waongeze bidii kwenye masomo ili baadaye waweze kulisaidia taifa kwenye Nyanja mbali mbali sambamba na wao kujiajiri huku akiwaonya waepuke makundi ya wahuni kutotumia madawa ya kulevya nao wasichana wasiingie kwenye vishawishi vitakavyochangia wapate ujauzito.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mhandisi Mshamu Munde alisema wamejipanga kukabiliana na changamoto kwenye sekta ya elimu inayochangiwa na ongezeko la wananfunzi kufuatia wazazi kuhamia kutoka Mikoa mbalimbali na uwepo wa viwanda vingi.
Munde alitumia fursa hiyo kuwataa watendaji wa vijiji hadi kata kutumia vikao vyao vya kisheria kuhamasisha wazazi wachangie kwenye madawati hatimaye ichochee ufaulu kwenye shule za awali, msingi hadi sekondari.
Naye mkuu wa shule hiyo Maritn Chuwa alipongeza Halmashauri ya Wilaya kufatilia kwa karibu katika kuboresha shule hiyo kongwe Wilayani humo huku akiahidi kushirikiana na walimu wenzake kuwafundisha kwa bidii wananfunzi wawe na matokeo mazuri
Hafla hiyo ilihudhuriwa na wakuu wa idara, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na serikali ya kijiji.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.