Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kwa ushirikiano na wadau mbalimbali wameadhimisha siku 16 ya kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu sambamba na siku ya msaada wa kisheria.
Madhimisho hayo yamefanyika jana kwenye viwanja vya stendi mpya ya Mwandege na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Takukuru, Paraligal, Repssi, Hdo na Dawati la Polisi Mkuranga.
Akizungumza kwenye hafla ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto na wiki ya msaada wa kisheria Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Arafa Halifa ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Usafi wa Mazingira na udhibiti wa taka
Kwa upande wake Mkuu wa Polisi wilayani Mkuranga Mratibu Mwandamizi Magai Chassa amesema vitendo 59 vya ubakaji, Kulawiti 27, Mimba 36 kwa Wanafunzi, shambulio la aibu 22 na kutelekeza family 3 vimeripotiwa kwa kipindi cha Januari hadi Desemba Mwaka huu.
Magai aliweka bayana kuwa matukio hayo yapo hatua mbalimbali za kisheria ili kupunguza na kukomesha vitendo hivyo kwenye vijiji 125 vya vilivyopo Wilayani Mkuranga.
Aidha kiongozi huyo alizitaja changamoto zinazowakabili ni ukosefu wa Ofisi za Dawati la jinsia kwenye Vituo vya polisi sambamba na ushirikiano duni na waathirika, Mila na desturi potofu na kesi nyingi kuzimalizia Nyumbani
Akiwahutubia wananchi uwanjani hapo Diwani wa Kata ya Mwandege kwa Niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Khadija Nasri Ali amewataka wananchi kufanya tathmini ya Ukatili na athari zake kisha kuziweka wazi katika vyombo husika hatimaye kuwe na Taifa Bora.
Aidha Mku huyo alizipongeza Taasisi kwa kuisaidia serikali katika mapambano hayo huku akiwataka viongozi na wazazi kutokufumbia macho vitendo hivyo
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.