Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yaadhimisha Siku ya Ukimwi Duniani tarehe 01/12/2022 katika Kijiji cha Shungubweni Wilayani Mkuranga na kuweka mpango madhubuti wa kuhakikisha agenda ya Ukimwi inakuwa ya kudumu katika Vikao na Mikutano Mbalimbali katika ngazi ya wilaya hadi Vitongoji.
Katika Maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya amesema wakati sasa umefika wa wazazi na walezi kutoa elimu ya Ukimwi kwa watoto wetu kwa uwazi na siyo kwa kuficha ili watoto watambue namna ya kujinginga na ugonjwa huu.
Akiwasilisha taarifa ya ukimwi Mratibu wa Ukimwi Wilaya ya Mkuranga Bi. Ana Molenga amesema Wilaya ya Mkuranga imeweza kupunguza kiwango cha maambukizi mapya kwa ujumla kutoka 3% Mwaka 2021 na kufika 2.8% Novemba mwaka 2022.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mohamed Mwela amemshauri Mkurugenzi kuwapa maelekezo Watendaji wa Vijiji kutenga Bajeti itakayowezesha kutimiza lengo la kutoa elimu dhidi ya Ukimwi katika vijiji vyao.
Maadhimisho hayo yalihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Khadija Nasri Ali, katibu Tawala, Mwenyekiti wa Halmashauri na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bi. Mwantum Mgonja.
Wengine ni Wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Wilaya pamoja na wadau na wataalam mbalimbali kutoka ndani ya wilaya ya Mkurnga.
Kauli mbiu ya Mwaka huu katika Maadhimisho ya siku hii ni IMARISHA USAWA.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.