Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Machi 5, 2024 imefanya maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani katika kata ya Mwarusembe.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika ofisi ya Kata/Kijiji cha Mwarusembe na kuhudhuriwa na Wananchi, Watumishi, Waheshimiwa madiwani na viongozi wa asasi mbalimbali.
Akizungumza kwenye shughuli hiyo, mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amewashukuru wakina mama wote waliojitokeza na kuwaambia Kwamba siku ya Mwanamke duniani ni siku ambayo wanawake wote hukutana kujadili na kupanga mikakati yao mbalimbali ya harakati iliyo asisiwa na wanawake wachache waliopigania uhuru na mafanikio yao licha ya changamoto walizokumbana nazo.
Vile vile amewaasa Wanawake washirikiane kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo ili waweze kufanikiwa kwa pamoja kwani mafanikio ya wengi yanapunguza mzigo kwenye jamii zao.
Aidha amewashauri Wanawake watangulize upendo mbele na utii katika yale yote wanayokwenda kuyafanya na kuyawekea mikakati ili yaweze kufanikiwa na kuondoa dhana potofu kwamba “adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzake”, lakini waende na kauli mbiu ya kwamba “rafiki wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe”.
Nae Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mohamed Mwera akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo, amewataka wanawake wote wasikusanyane bali washikamane na kushirikiana kwenye shughuli zao mbalimbali za kimaendeleo ili waweze kutimiza malengo yao pamoja.
hafia hiyo imeenda sambamba na ugawaji wa misaada kwa wazee wenye uhitaji katika vitongoji viwili, Kitongoji cha Mwarusembe mjini na Kitongoji cha Uzizi kijiji cha Kitonga.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.