Wilaya ya Mkuranga, imeanza rasmi zoezi la kutoa vitambulisho vya ujasiriamali kwa wafanyabiashara ndogondogo ikiwa ni zoezi lililoasisiwa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli
Akizindua zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya godown wilayani hapa, Mkuu wa wilaya ya Mkuranga Mh. Filberto Sanga, alikemea vikali wale wadanganyifu wataojitokeza kufanya ulaghai ili kupatiwa vitambulisho hivyo kinyume na utaratibu “Kusiwepo na udanganyifu na atakaebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria” alisisitiza Sanga
Sanga aliongeza kuwa, wanufaika wa vitambulisho hivyo ni wafanyabiashara ndogondogo ambao mapato ya faida yao hayazidi Tsh Milioni 4 kwa mwaka na kwa kuanza wilaya itatoa vitambulisho kwa wajasiliamali 265 ambao wamehakikiwa na kukidhi vigezo huku maombi mengine yakiendelea kuhakikiwa.
Zoezi hilo pia lilihudhuriwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga Eng. Mshamu Munde, Maafisa wa TRA, Mkuu wa jeshi la Polisi wilaya, Madiwani, pamoja na Viongozi wa chama cha mapinduzi (CCM)
Kwa upande wa baadhi ya wajasiriamali wilayani Mkuranga wamepongeza kuwepo kwa zoezi hilo na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kuwaangalia wajasiriamali, wafanyabiashara ndogondogo kwa jicho la tatu ili kutambulika na kujiongezea kipato.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.