Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imevuka lengo katika kutekeleza zoezi la chanjo ya POLIO kwa watoto wenye umri chini ya miaka 5 baada ya kufanyika kw a zoezi hilo katika kipindi cha awamu tatu.
Hayo yamesemwa leo tarehe 24/11/2022 na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Veronica Kinyemi katika kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi Kilichofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga.
“Katika utoaji wa chanjo awamu ya tatu tulitegemea kuwafikia watoto wote chini ya miaka kitano 47044 waliopatiwa chanjo katika awamu ya pili lakini wakati wa utekelezaji wa utoaji wa chanjo tukawafikia watoto 54249 sawa na 115% zaidi ya lengo kusudiwa” Katibu Tawala alisema.
Kikao hiko kimefanyika kwa lengo la kuhamasisha wajumbe na wadau mbali mbali ili waweze kwenda katika jamii na kuhamasisha na kufanya utekelezaji wa zoezi la chanjo ya UVICO - 19 ambalo limeanza tarehe 24 na kuisha tarehe 30 Mwezi Novemba sambamba na zoezi la chanjo ya POLIO ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 1 hadi tarehe 4 Mwezi Desemba Mwaka huu.
Aidha Bi. Veronica ametaka zoezi la chanjo ya uvico - 19 kwa sasa likatekelezwe kwa uhakika na ikibidi zoezi hilo lifanyike Nyumba kwa Nyumba ili kuhakikisha kila mwana Mkuranga awe amefikiwa na huduma hiyo.
Nae Afisa afya wa Wilaya Angelus Mtewa kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga akijibu baadhi ya maswali ya wajumbe amesema kuwa kuna changamoto nyingi katika zoezi hili hasa kwa baadhi ya wananchi kuipotosha jamii.
“hii chanjo ni salama kwa Mwanadamu kama huduma nyingine za chanjo zinazotolewa katika hospitali na Vituo vya kutolea huduma hizo , hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha tunaenda kutoa elimu kwa usahihi ili jamii ielewe umuhimu wa chanjo hizi.” alisema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga akiwakilishwa na Afisa Mazingira na Usafi Bi. Arafa Halifa amewataka Viongozi wa dini zote ndani ya wilaya ya Mkuranga kuendelea kuhamasisha zoezi hilo la chanjo katika maeneo yao ya ibada.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.