Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe. Khadija Nassir Ali amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kusimama sekta ya Kilimo kwa kuleta ruzuku ya pembejeo na kufungua milango kimataifa hali inayochangia wanunuzi kujitokeza kwa wingi na kuboresha bei za nafaka.
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amesema hayo akizungumza kwenye mnada wa ufuta Mkoa wa Pwani uliofanyika katika Kijiji cha Kingoma Wilaya ya Mkuranga huku akiwaonya wakulima kutorubuniwa na kuuza Ufuta kwa walanguzi ili kutokwamisha juhudi za Rais.
Kiongozi huyo aliweka wazi wamejipanga usiku na mchana kuwadhibiti watoroshaji na kuchukua hatua kali kama fundisho na amewataka wakulima kuonyesha shukrani kwa Rais kwa kutumia malipo yao kwa kujenga nyumba bora na kusomesha watoto hadi elimu ya juu.
Aidha amewataka viongozi wa (AMCOS) kutoa malipo ya wakulima ndani ya siku saba baada ya mnada huku akimpongeza Mwenyekiti wa (CORECU) Mussa Ngereza na viongozii wenzake kwa kusimama vizuri kwenye nafasi zao kwa kuboresha hali za wakulima mkoa wa pwani.
Mnada wa ufuta Mkuranga kwa awamu hii ya kwanza imefanikiwa kuuza tani elfu 155 sawa na Kilo Laki 1.5 ambapo Kampuni (20) zimejitokeza kwenye mnada huku bei ya juu baada ya kuchakata ikiwa ni Tsh. 3,951.90 ambapo wakulima waliridhia.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.