Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Philberto Sanga amepokea msaada wa vifaa kinga kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa homa ya mapafu-CORONA- kutoka Kampuni ya FUJIAN inayojishughulisha na uundaji wa nondo kilichopo Kisemvule wilayani Mkuranga.
SANGA amesema vifaa hivyo vimefika wakati muafaka na kuwataka viongozi na wataalam kuhakikisha wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi na kusambaza vitakasa mikono hivyo katika maeneo mbalimbali sambamba na kuwataka wananchi kutekeleza maelekezo ya wataalamu wa Afya ni jinsi gani wanaweza kujikinga na ugonjwa huo wa CORONA.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Fujian Xu Xingda amewashukuru viongozi wa Wilaya kwa kumshirikisha katika mapambano haya sambamba na kumshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuisimamia vema sekta ya viwanda na kusema malengo ya kutoa msaada huo kwa Wilaya ya Mkuranga ni kuunga mkono jitihada za serikali dhidi ya ugonjwa huo.
Pamoja na kupokea vifaa hivyo pia uongozi wa Mkoa wa Pwani umetoa mavazi maalum 11 kwa ajili ya wahudumu watakaotoa huduma kwa wagonjwa pindi watakapotokea sambamba na kutenga maeneo kwa ajili ya wananchi watakaopatikana na ugonjwa huo ili kupatiwa huduma.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mkuranga Ally Msikamo akitoa neno la shukrani amesema wanashukuru kwa kupatiwa vifaa kinga hivyo na kuwataka wadau wengine kufanya hivyo, “Ukisikia mtu anakushukuru ujue anataka tena” hivyo kama kuna vingine tuletewe tuu kwani hatujui ugonjwa huu utaisha lini.
Kampuni hiyo imekabidhi ndoo maalum 100 za kuririsha maji na sabuni chupa 140 ikiwa ni mwanzo na kuahidi kuendelea kufanya hivyo mara tu baadhi ya vifaa vilivyopo njiani kufika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.