Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewataka wananchi wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kuchangamkia fursa ya Nyuki ili waweze kujikwamua kiuchumi sambamba na kuboresha afya zao.
Akizindua kampeni hiyo juzi kwenye ukumbi wa Flex Garden Kiguza, Ulega ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mkuranga aliwahakikishia Wanavikundi na kitengo cha Njuki kutatua changamoto zinazokwamishamkakati huo endelevu hatimaye mauzp ya nyuki yalete tija kwao na kuongeza mapato ya Halmashauri ya wilaya.
Ulega aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alikabidhiwa tuzo ya shukrani huku mkuu huyo akimwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Mhandisi Mshamu Munde kuhakikisha hotuba ya uzinduzi huo wanasambaziwa Madiwani, Watendaji na wataalam ili elimu iwafikie wananchi Vijijini .
Akitoa salamu za Mkoa, Afisa Maliasili Mkoa Pierre Ntiya Magwa alisema mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ameipongeza Halmashauri ya Mkuranga ambayo ni pekee kwa Mkoa kuzindua kampeni ya fursa za nyuki, sambamba na wiki iliyopita kuzindua “Mkuranga tokomeza utapiamlo lishe bora kwa watoto chini ya miaka mitano” hivyo Ndikilo aliziagiza Halmashauri nyingine kuiga ubunifu huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri Mhandisi Mshamu Munde aliwapongeza wadau mbalimbali waliowaunga mkono katika Kampeni hizo huku akimhakikishia Mbunge Ulega kumpa ushirikiano katika kufanikisha kampeni hiyo ambavyo inalenga kuongeza thamani mazao ya Nyuki sambamba na kutafuta masoko ya uhakika.
Mmoja wa wanufaika wa tuzo za shukrani Victor Ngalla, Meneja mauzo na masoko katika Kampuni ya Bakhressa aliwahakikishia washiriki kutumia uzoefu wake kupata masoko ndani na nje ya Nchi.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.