Akiongea ofisini kwake leo, Mkurugenzi Mtendaji (w) Mhandisi Mshamu A. Munde alisema, baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika Hospitali ya wilaya alisikitishwa mno na kasi ndogo ya utoaji wa huduma katika Maabara ya Hospitali hiyo. Kutokana na hali hiyo amemwagiza Mganga mkuu wa hospitali hiyo Daktari Stephen Mwandambo kufanya yafuatayo:-
1. Kusimamia kwa karibu huduma katika kitengo cha maabara ili kuongeza kasi ya Upimaji na kutolewa kwa majibu kwa wagonjwa ili kuondoa msongamano na kutumika kwa muda mrefu kusubiri vipimo.
2. Kuainisha mahitaji muhimu na kuwasilisha taarifa jumatatu tarehe 15.01.2018 saa 2:00 asubuhi
3. Kupanua huduma ya upimaji kwa kuongeza vyumba vya kuchukulia sampuli.
4. Kuandaa mpango wa muda mrefu wa uboreshaji wa huduma za afya hospitalini hapo na kuuingiza katika bajeti kuu ya Halmashauri.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.