Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mkuranga Mwantu Mgonja leo amekabidhi jumla ya Vyumba vya Madarasa 132 kwa Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali ikiwa ni ishara ya kupokea wanafunzi wapya wa kidato cha kwanza mwezi Januari 2023.
Mwantum amekabidhi Madarasa hayo katika hafla iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Kazole Kata ya Vikindu Tarafa ya Mkuranga ambapo Mkuu wea Wilaya alikabidhiwa Madarasa sit ikiwa ni miongoni mwa Madarasa 132 yaliyojengwa.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imefanikiw kujrenga Vyunba vya Madarasa 132 baada ya kupata fedha kiasi cha shilingi Bilioni 2.64 kutoka Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha baada ya kupokea Madarasa hayo Mkuu wa Wilaya Ya Mkuranga amempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri na wataalamu wake kwa kusimamai vema Ujenzi huo na kusema kuwa ameridhishwa na spidi pamoja na viwango katika kutekeleza kazi hiyo.
Sambamba na hili Bi. Khadija ameagiza kwa wakuu wote wa shule kushirikiana na tfs ili kupata Miche ya miti na kuwapa wanafunzi wa kidato cha kwanza waeze kupanda ili kuasisi kauli ya Mh. Rais ya utunzaji wa Mazingira sambamba na kuilinda miundo mbinu ya Majengo hayo.
Pamoja na Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza wazazi wote ambao watoto wao wamebahatika
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.