Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Mwantum Mgonja akiongozwa na timu maalum ya wataalam wamefanya kikao kazi pamoja na kukagua Mradi wa shule mpya ya Sekondari ya Shungubweni fedha kutoka Serikali Kuu shil.Mil 600.
Katika kikao hicho amewaeleza wanakamati kuhakikisha makubaliano yote yanayofanyika yawe katika mfumo wa maandishi ili kuepuka sitofahamu ambayo inaweza kuibua mgogoro .
Pia amewashukuru kamati ya usimamizi wa ujenzi wa shule hiyo kwausimamizi mzuri wa mradi huo umefika katika hatua nzuri na kuahidi kuzidi kushirikiana nao kwa karibu mpka mradi huo utakapokamilika.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.