Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga limeketi na kufanya Mkutano Maalum wa kujadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) kwa Mwaka wa fedha 2021/2022 unaoishia Juni 2022.
Katika taarifa hiyo, kwa Mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 juni 2022 Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali CAG zinaonesha alikagua hesabu za Serikali za Halmashauri na kutoa hati inayoridhisha (hati Safi) ya ukaguzi, hali hii imepelekea mwenendo wa Halmasauri kupata hati safi za ukaguzi kwa miaka (7) Mfululizo kuanzia mwaka 2015/2016 hadi 2021/2022.
Akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mkuranga, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge ameiagiza menejimenti kumaliza hoja zote ambazo ziko ndani ya uwezo wa Halmashauri isipokuwa hoja ambazo zinategemea maamuzi ya Serikali na hoja hizo ziwasilishwe ofisini kwake kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi.
Nae Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Rashid Kassim Mchatta amewataka watumishi kutoa taarifa kwa viongozi wa juu mara zinapoitajika na baadae kutoa taarifa hizo kwa kiongozi wake wa karibu ili kufanikisha uharaka uliopo na kuwezesha viongozi wetu kufanya kazi kwa ufanisi na uharaka.
Awali Mkuu wa wilaya ya Mkuranga, Khadija Nassir Ally amemtaka Mwenyekiti wa Halmashauri kwenda kusimamia namna ya uhamishaji wa watumishi haswa kwa watendaji wa vijiji, kwani husababisha madeni mengi ambayo yanakwenda kutengeneza hoja za CAG.
“………. Lakini ukikaa na Afisa Utumishi ukimuuliza hivi kulikuwa na sababu gani mtendaji huyo kuzunguka vituo vitatu katika miezi sita (6) sababu zitazokuwa ni kwa sababu, inawezekana sisi viongozi wa kisiasa ndiyo tumeomba na tumeshindwa kufanya nae kazi kwa maslahi yetu, hiyo ndiyo sababu kubwa huwa ninayoipata ninapouliza….” Alisema Mkuu wa wilaya.
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga ilikuwa na hoja 66 ambapo hoja 30 ni za miaka ya nyuma na hoja 36 ni za mwaka wa Fedha uliokaguliwa 2021/2022, na kati ya hoja hizo Halmashauri imezifanyia kazi jumla ya mapendekezo 41 ambazo tayari zimefungwa kabisa na kusalia hoja 25.

Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.