Mbunge wa Jimbo Mkuranga ambaye pia ni waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Abdallah Ulega amefanya Mkutano wa kufunga Mwaka 2023 kwa kugawa Vifaa vya Ujenzi kwa ajili ya kuendeleza miradi ya wananchi pamoja na kugawa Boti 4 kwa wavuvi bila ya kusahau na mashine za kufyatulia tofali.
zoezi hilo la ugawaji wa vitu hivyo lilifanywa na Mgeni rasmi Mh. Rabia Abdalla Hamid Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI) lilifanyika katika eneo la Mkutano ulifanyika katika viwaja vya Shule ya Msingi Mkuranga.
katika Mkutano huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh. Abubakari Kunenge ulikuwa na lengo la kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Miradi ya serikali ya awmu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndani ya Wilaya ya Mkuranga pamoja na kusikiliza na kutatua kero za wananchi
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.