Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga kwaajili ya kukagua miradi ya maendeleo ambayo Mwenge unatarajiwa kupita.Kunenge amefanya ukaguzi huo kujiridhisha ujenzi wa miradi hiyo siku chache kabla ya mwenge kufika katika mkoa wa Pwani.
Akiwa katika miradi hiyo Kunenge amesema ipo ambayo imetekelezwa kwa fedha za Tozo hivyo kukamilika kwake inaonyesha ni namna gani tozo zimesaidia kuondoa vikwazo kwa wananchi.
Aidha amezitaka Taasisi zinazotoa huduma za jamii ikiwemo Tanesco na Ruwasa kufikisha maji na umeme kwenye mradi wa kituo cha afya Msolwa ili kitakapoanza kutumika kisiwe na vikwazo.
Amewaagiza pia wataalamu kutekeleza majukumu yao kikamilifu ili miradi inayotekelezwa iweze kukamilika kwa wakati na kwa kiwango kinachotakiwa.
Mwenge wa Uhuru unatarajiwa kupokelewa katika mkoa wa Pwani mwanzoni mwa mwezi Mei.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.