Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Aboubakar Kunenga amewataka wazazi wa Mkoa wa huo kuhakikisha wanafunzi waliofaulu kuingia kidato cha kwanza wote wanaenda shule ifikapo January 17,2021.
Akizungumza wakati wa ukaguzi wa miradi ya elimu iliyojengwa kutokana na fedha ambazo Serikali imeupata kutoka Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) kwa ajili ya kupambana na athari za UVIKO-19 na kuzielekeza kuimarisha huduma za jamii alisema kuwa hakuna mzazi anayeruhusiwa kukaa na mtoto bila kupelekwa shule labda kama anachangamoto za kiafya zilizothibitishwa na wataalamu wa afya.
Sambamba na hilo Mhe.Kunenge amempongeza namna ambavyo Mkuu wa Wilaya na Timu kutoka Ofisi ya Mkurungenzi kushikana bega kwa bega hatimaye kupelekea madarasa yote 146 kukamilika kwa wakati Pamoja na kuwepo changamoto za miundombinu zilizopelekea baadhi ya sehemu kuendesha shughuli za ujenzi kwa kususua.
Jumla ya vyumba 535 vya madarasa vimejegwa katika Mkoa wa Pwani ,kati ya hiyo 146 vipo ndani ya Wilaya ya Mkuranga na vyote vipo tayari kupokea wanafunzi ifikapo Januari 17 Mwaka huu.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.