Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Aboubakar Mussa Kunenge ameshirika katika halfa ya makabidhiano ya majengo ya madarasa na ofisi yaliyofadhiliwa na shirika la Direct Aid Society Tanzania. Halfa hiyo imefanyika katika kijiji cha Mwanambaya katika Kata ya Mipeko Wilaya ya mkuranga.
Mhe. Aboubakar Mussa Kunenge ambae ndie mgeni rasmi katika halfa hiyo amewashukuru sana Taasisi hiyo kwa kuweza kujenga madarasa kwaajili ya walemavu wasiona ili waweze kujifunzia elimu ya Dini ya kiislamu kwani serikali ipo pamoja nao katika kushirikiana kwenye kuleta maendeleo katika jamii zinazotuzunguka.
Pia amewataka walemavu hao wa macho kuzingatia elimu watakayopewa na walimu hao na kuwapa heshima walimu hao kwani ndio elimu hiyo ndio msingi imara utakaoleta mwangaza katika maisha yao kwa hapa duniani na kesho akhera
Aidha amewataka waumini wote wa kiislamu kuzingatia kufanya mema na wazidi kufanya ibada kwa sana na kuzidi kuliombea Taifa liwe na amani na kumuombea dua Rais wetu Mhe.Samia Suluhu Hassan.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.