Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe.Abubakar Kunenge amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwaleta wawekezaji kwenye sekta ya kilimo.
Akifungua kikao cha wadau wa Korosho ndani ya Wilaya Mkuranga Mkoani Pwani katik ukumbi wa Flex Garden Kiguza Mhe.Kunenge amemuhakikishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wametekeleza maagizo yake ya kubangua korosho ndani ya Mkoa.
Aidha Mhe.Kunenge aliendelea kumpongeza Rais kwa kuwaletea wakulima mbolea ya ruzuku ambayo itachangia Mkoa kuongeza ubora wa korosho aidha amewataka wakulima waangalie mnyororo wa thamani kwa lengo la kuzalisha tani za kutosha msimu huu huku Korosho daraja la kwanza ifikie asilimia 72%.
Pia amewataka wakulima kusafisha mashamba na kuwaagiza Wakuu wa Wilaya zote wa Mikoa ya Pwani kuhakikisha wakulima wanaachana na utamaduni wa kuchoma mashamba ya korosho.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amewataka Maofisa Kilimo wahakikishe wanapata takwimu za wakulima na idadi ya mikorosho huku wakijapanga kutatua changamoto ya ugawaji pembejeo kwa walegwa huku akiwa sambamba na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kukomesha utoroshaji wa korosho na ununuzi batili kupitia Kangomba.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.