Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga amewaagiza watendaji wa Kata wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani kutoa maelekezo kwa wananchi kutowaruhusu watoto wao kwenda shule kwa kipindi chote ambacho mvua zitakuwa zikinyesha katika kipindi cha masika na mvua za vuli na kusababisha mabonde mengi kupitisha maji kwa kasi.
Sanga ametoa agizo hilo mwanzoni mwa wiki hii katika Mkutano kazi wa Kuwapa maelekezo ya utendaji wa shughuli za Serikali kwa Wenyeviti Vijiji na Vitongoji katika ukumbi wa Sekondari ya Mwinyi Mkuranga na kusisitiza ni bora kuvumilia mvua zipite kuliko kupoteza watoto katika kipindi hiko ambacho ni mara nyingi watoto wanakufa kutokana na kusombwa na maji yanayopita katika mito mbalimbali wakati wa kwenda na kurudi shule.
Aidha amewataka viongozi hao kwenda kuwasaidia wananchi bila ubaguzi wa kuangali kabila la mtu, rangi, dini au vyama na wahakikishe wanaenda kutatua migogoro iliyopo kwa wananachi sambamba na kuacha kutumia madaraka yao vibaya ambapo amewaahidi endapo wataenda kinyume na taratibu hawatosita kuwanyang’anya kadi kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kuwaondoa katika nyafazi zao.
Akijibu baadhi ya maswali kutoka kwa viongozi hao Sanga amesema katika changamoto ya Barabara ambazo zimeharibiwa na mvua hivi karibuni, tayari mkandarasi ameshapatikana na tayari mikataba ya kufanya kazi hiyi imeshasainiwa isipokuwa wanasubili hali ya mvua itulie ili ukarabati wa miundo mbinu hiyo ifanyike.
Akihitimisha Mkutano huo Sanga amewaambia Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji kuwa hawakuchaguliwa kwa ajili ya kwenda kuuza Ardhi bali kuwasimamia wananchi katika mahitaji yao kama ambavyo Rais John Pombe Magufuli anataka na kama wanaona hawatoweza basi waachie ngazi mapema sambamba na kuiagiza Takukuru kufanya uchunguzi katika vijiji vyote vinavyofanya mauzo ya Ardhi ili kubaini fedha zilizokusanywa zimetumikaje.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Mhandisi Mshamu Munde amewataka wamiliki wote wa machimbo ya mchanga kufanya marekebisho ya barabara wanazotumia kupitisha magari yao kwani imekuwa kero kwa wananchi kushindwa kupita na magari madogo kutokan na uhharibifu unaofanywa na magari hayo.
Viongozi hao wa Vijiji wameingia makubaliano kuwa wako tayari kuwajibishwa itakapotekea kuulizwa maswali matano katika mikutano itakayofanywa na Mkuu wa wilaya katika ziara zake vijijini.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.