Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amewayaka wananchi wa kijiji cha Kerekese kilichopo Kata ya Kisiju kushiriki zoezi la Semnsa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23,2022.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijijini hapo Mhe.Hadija Nasri Ali amewaelezea wananchi umuhimu wa kushiriki kwenye zoezi la sensa ili kuwezesha serikali kuwa na takwimu sahihi za idadi ya watu na kuweza kuwapangia mipango ya maendeleo inayoakisi hali halisi.
Sambamba na hilo kiongozi huyo amewataka wafugaji wavamizi kutoa taarifa kwa viongozi wa vijiji ili kuwapa utaratibu wa kutunza mifugo yao pasipo na kuingilia shughuli za wakulima na kusababisha hasara na uharibifu wa mazao.
Aidha Diwani wa Kata ya Kisiju Bw.Ally Mohamed Dau amewaomba wananchi wa Kerekese kushiriki katika ujenzi wa miradi ya maendeleo ikiwa pamoja na kusimamia vifaa vya ujenzi wakati wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.