Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Mhe.Hadija Nasri Ali ameitaka mahakama ya Ardhi kuendelea kutoa Msaada wa Elimu juu ya uendeshaji wa kesi za zinazohusu ardhi hii ni kutokana na kuwepo kwa malalamiko mengi kwa wananchi juu ya kesi hizo kwa sababu ya kukosa uelewa wa namna zinavyoendeshwa.
“Katika kesi nyingi zinazofika katika ofisi yangu zinahusiana na ardhi na kwa vile ni eneo linalo lalamikiwa kwa wingi sana basi naendelea kutoa maelekezo kwa wahusika wote lakini pia kuwashauri kuendesha mashauri hayo kwa haraka ili wananchi waweze kupata haki zao na kufurahia uwepo wa Serikali ndani ya maeneo yao” Alisema.
Akizungumzia umuhimu wa Teknolojia Mahakamani Hakimu Mfawidhi Wilaya Herieth Mwailolo amesema Mahabusu wengi wamefurahia matumizi ya uendeshaji wa kesi kimtandao hii ni kwa sababu inapunguza kuhairishwa kwa kesi pia kesi zinafikia hukumu kwa wakati na kwa mda mfupi.
Akiongezea umuhimu wa mahakama ya kimtandao Emanuel Maleko Wakili Mwandamizi wa Serikali Mkoa wa Pwani amesema tumeshuhudia matumizi ya mtandao kusajili na kusikiliza mashauri yakifanikisha usimamizi na utoaji haki hasa katika kipindi cha janga la UVIKO 19 ambapo mashauri yalisikilizwa bila msongamano mahakamani, kwa mfano katika mashauri ya jinai watuhumiwa walisomewa mashitaka na mashauri kuendeshwa wakiwa mahabusu na rufaa kusikilizwa huku wafungwa wakiwa magerezani.
Aidha , Mfumo wa Mahakama Mtandao umeleta faida kubwa ikiwa ni pamoja na kuokoa muda na gharama za Makatibu Sheria na Mawakili wa Serikali pamoja na wadau mbalimbali kusafiri katika wilaya na mikoa mbalimbali kusajili na kuendesha mashauri, kuongeza uwazi na kutoa huduma kwa ufanisi. Aliongeza.
Naye Majid Matitu wakili wa kujitegemea na mwakilishi wa Chama cha Mawakili
Tanganyika (TLS) Pwani ameeleza changamoto zinazowakabili ni Mawakili Vishoka pamoja na baadhi ya ofisi za Serikali na Taasisi za Fedha kuwarudisha wananchi wanaowaandalia nyaraka za kisheria katika kupata huduma na kuwarejesha kwa kuwaeleza kuwa ni lazima zigongwe muhuri wa mahakama tu.
Maadhimisho yalipambwa kwa kauli mbiu isemayo
"ZAMA ZA MAPINDUZI YA NNE YA VIWANDA SAFARI YA MABORESHO KUELEKEA MAHAKAMA MTANDAO".
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.