Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali amekutana na wakulima wa zao la korosho katika zoezi la Parizi ya Korosho katika kitongoji cha Mitoboto kilichopo katika kijiji cha Mwarusembe .
Katika zoezi hilo Mhe.Hadija Nasri Ali alizungumza na wananchi wa kitongoji hicho na kusema kuwa tunahitaji kukiinua kilimo chetu cha korosho hivyo tunatakiwa kufata taratibu zote za kitaalamu ikiwemo kuparizi na kupulizia dawa mashamba yetu ili tuweze kupata matunda mazuri na tufikie malengo yetu.
Pia amesema katika Wilaya ya Mkuranga tuna korosho bora licha ya changamoto mbalimbali zilizojitokeza hapo nyuma ndio zilizosababisha kurudisha nyuma kilimo hicho hivyo amewataka wananchi kushirikiana na viongozi pamoja na wataalamu kwenye kuzalisha zao hilo lirudi kwenye ubora wake kama hapo Awali lilivyokuwa.
Aidha,amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kuleta Salfa pamoja na dawa zote muhimu za kilimo cha korosho venvye thamani ya shilingi bil.20 kwa Mko wa pwani hivyo ameahidi kuweka utaratibu mzuri wa kuhakikisha mkulima anapata.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Bi.Anna Kiria amewataka wadau wa kilimo cha Korosho kuleta vifaa kwa wakulima kwani wakulima hao wanauhitaji wa vifaa na wanatakiwa kuweka utaratibu ambao hautomuumiza mkulima.
Pia amewasihi wakulima kwenye kupalilia na kupulizia dawa mashamba yao ili kuweza kupata korosho zenye ubora wa grade A ili tukuze soko letu na Halmashauri yetu iweze kupata mapato mazuri ya ndani kupitia zao hilo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.