Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nasiri Ally amabe ni Mwenyekiti wa kamati ya maendeleo ya Wilaya (DCC) amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Bi Mwamtumu Mgonja kuhakikisha kuwa yeye na wakuu wa idara wanahudhuria kwenye vikao vyake badala ya kuwaagiza makaimu wao kwani uwepo wao unaumuhimi mkubwa wa kuleta tija kwenye mkutano huo ambao ni kiungo kuelekea kikao cha Mkoa akizungumza hayo wakati wa mkutano wa kamati ya maendeleo ya Wilaya hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Flexi.
Pia ameelezea mafanikio ya miradi ya maendeleo ambapo amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia sh,Bilioni 2.7 ambazo zipo nje ya pesa za Bajeti zilizopitishwa na Bunge kwa ajili ya maendeleo, ameahidi kuzisimamia pesa hizo usiku na mchana kwenye matumizi sahihi ya miradi ambayo itatekelezwa kupitia pesa hizo .
Kwa upande wake Mhifadhi Misitu (TFS) Wilaya ya Mkuranga Charles Kaselya aliwaomba TARURA na TANROAD kuboresha barabara ya Kisiju Pwani ambayo inaunganisha kijiji cha Shungubweni(Boza) ambapo kuna fursa za utalii kwani watalii wengi wanashindwa kufika kutokana na miundombinu mibovu ya barabara hiyo na wakati mwingine watalii wakifika wanakuwa wamechoka sana.
Akiwasilisha taarifa ya pesa Mtunza Hazina wa Halmshauri ya Wilaya alisema wameweza kukusanya sh.Billioni 42,177,766 mwaka 2021/2022 wakati wa kazi ya utekelezaji wa Bajeti 2021/2022 ukiwa unaendelea .
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.