Mkuu wa Utawala Jeshi la Polisi DCP Anthony J. Ruta amefungua Ofis ya Kikosi cha Usalama Barabarani ambayo ipo ndani ya kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mkuranga .
DCP Anthony J. Ruta amepongeza juhudi nzuri za kazi zinzofanyika na kikosi hicho cha usalama barabarani kwa kuweza kujenga jengo hilo hivyo amewataka kuzidi kusimamia vyema sheria za usalama barabarani ili kuweza kupunguza ajali barabarani.
Aidha amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mhe.Hadija Nasri Ali ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama ya Wilaya kwa usimamizi mzuri na michango anayotoa katika kikosi hicho cha usalama barabarani hvyo amemsisihi kuzidi kuendelea kutoa michango.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255222928730
Simu ya Mkononi: 0634329394
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2026 MkurangaDc. All rights reserved.