Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani Khadija Nasri Ali amewapongeza wataalamu, Watendaji na Madiwani kwa kusimamia ukusanyaji wa mapato sambamba na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Akizungumza kwenye Baraza la Madiwani robo ya pili mwaka 2020/2021 0ktoba-Desemba Khadija aliwahakikishia Madiwani kuongeza nguvu katika kudhibiti mianya kwenye ukusanyaji wa mapato.
Aidha aliwaagiza Madiwani, Watendaji na Wataalam kusimamia maagizo ya Serikali ya utekelezaji wa Anuani za makazi na Sensa, sambamba na kuchanja ili kujilinda na UVIKO-19.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi ambaye ni mbunge Abdalla Ulega ameahidi kufikisha ngazi za juu ombi la ujenzi wa Hospital Mpya ya Wilaya , Kijiji cha Mwarusembe kama utekelezaji wa ahadi ya Waziri wa (TAMISEMI) wa zamani Ummy Mwalimu alipotembelea Mkuranga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri Mwantumu Mgonja aliomba ushirikiano wa dhati na Madiwani katika kusukuma gurudumu la maendeleoili madiwani wawe na Kazi rahisi Mwaka (2025).
Awali Madiwani walishiriki kikao cha Baraza kuwasilisha taarifa za utekelezaji kata zote 25.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.