Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga yaadhimisha siku ya Mazingira Duniani katika eneo la soko kuu la Halmashauri.
Katika Maadhimisho hayo kumefanyika usafi wa nje ya Soko ukiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi. Hadija Nassir Ali alieambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri sambamba na Mkurugenzi Mtendaji.
Mhe.Hadija Nasri Ali ambae ndiye Mgeni Rasmi amezungumza na Wananchi na kusema “usafi ni muhimu hivyo tunawajibu wa kuhakikisha kuwa mazingira yanayotuzunguka yanakuwa safi na salama kwa afya zetu”.
Aidha amewataka Maafisa mazingira kufata Sheria,Kanuni na taratibu za kazi zao katika ukaguzi wa viwanda ambavyo vipo ndani ya wilaya na kusisitiza kuwa endapo kuna kiwanda ambacho hakifati sheria na taratibu zilizowekwa kisheria basi achukuliwe hatua ikiwemo kufungiwa shughuli za uzalishaji kiwandani hapo.
Sambamba na hilo, amesisitiza kupitiwa kwa Sheria ndogo za utunzaji wa Mazingira kulinga na wakati wa sasa ambapo ukuaji wa miji umekuwa mkubwa.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Bi.Mwantum Mgonja amewashukuru wananchi wote waliojitokeza katika kufanya usafi kwenye siku ya mazingira huku akiwaomba kuendeleza kutunza mazingira yanayowazunguka kwa kufanya usafi mara kwa mara
“ Mazingira ni Afya hivyo tunatakiwa kuyatunza”
Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga imeendelea kutekeleza maazimio ya kuhakikisha kila ifikapo Jumamosi ya mwisho wa mwezi usafi unafanyika kwenye maeneo yote.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.