Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Bi Khadija Nasiri Ally ameitaka michango ya Asasi za kiraia (NGO's) ijikite katika maendeleo ya Wilaya kubainisha changamoto na kuimarisha mahusiano kati ya serikali na NGO's zinazotoa huduma katika Wilaya hii.
Akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa masharika yasiyo ya kiserikali (NGOs') ,Mkuu huyo amesema sera ya Taifa ya NGO's mwaka 2001 imeweka misingi ya uratibu pamoja na mazingira wezeshi ya utendaji kazi .
Akizungumzia mkutano wa NGO's Taifa ambao mgeni rasmi alikuwa Rais Samia Suluhu Hassan ameelekeza mipango ya (NGO's) iangalie mipango ya kitaifa ,Mashirika yaongeze uwazi katika utendaji kazi ,wawe na mipango wa kujitegemea unaozingatia tamaduni. Nae Bi khadija amezitaka NGO's kufahamu mkono wa pili wa serikali ambapo mwongozo unazitaka zifanye shughuli zao kwa uwazi kama taarifa za fedha,ulipaji ada ifanyike kwa wakati .
Aidha taarifa ya Mkoa iliyowasilishwa na Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga Peter Nambunga amesema wanapokea maombi ya usajili kwa kujikita kwenye malengo na kuangalia matumizi ya pesa watazitambua NGO's wanaofanya nao kazi. Pia Bw.Nambunga alitumia fursa hiyo kuweka bayana Bajeti ya Halmshauri ifanyike baada ya kukutana na NGO's kazi za NGO's za Taifa zishirikishe zile ndogo ili kuwajengea uwezo.
Nae Mwanasheria wa serikali kutoka Wizara ya Afya !Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Faki Shaweji amezitaka NGO's ziwasilishe taarifa ya fedha robo mwaka kwa msajili ili kuwekea uhai wao.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye pia Mwanasheria wa Halmashauri amezitaka NGO's kutumia vikao vya Baraza la Madiwani ambalo la wazi kuangalia fursa zinazopatikana katika sekta ya elimu ,afya ,kilimo na zinginezo ili wafaidike na fursa zitolewazo.
Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga
Postal Address: P. O. Box 10, Mkuranga, Pwani, Tanzania
Telephone: +255232110038
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@mkurangadc.go.tz; ded.mkuranga@pwani.go.tz
Copyright ©2023 MkurangaDc. All rights reserved.